Ligi kuu ya NBC inatarajiwa kuendelea hii leo kwa michezo miwili ambapo mchezo wa jioni kabisa utakuwa ni kati ya KMC dhidi ya Namungo ambao utapigwa katika dimba la Majaliwa.
KMC ambayo inakocha mpya kwasasa walinusurika kushuka daraja msimu uliopita baada ya kuangukia plat-off ambayo walipita dhidi ya Mbeya City, japokuwa presha ilikuwa juu sana.
Namungo wao huu ni mchezo wao wa pili wa ligi kuu wanaenda kucheza baada ya kupoteza mchezo wao wa kwanza wa ligi dhidi ya JKT waliopanda daraja msimu huu.
Klabu hiyo ya Kinondoni kupitia kocha wao Mkuu Moalini wamesema kuwa wamejiandaa vizuri kuchukua pointi tatu kwenye mechi hii ya leo na watajitahidi kushinda mechi zao za ligi zinazofuata.
Mechi ya mwisho kukutana timu hizi mbili, Namungo alishinda mechi hiyo kwa kishindo. Je leo hii nani ataondoka na pointi tatu huko Lindi?