Mzunguko wa pili wa Ligi kuu ya NBC utaendelea kesho ambapo KMC itawakaribisha Coastal Union katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar.

KMC chini ya kocha Mkuu, Thierry Hitimana imekamilisha maandalizi ya mchezo huo na wachezaji wote wapo tayari kuanza vyema mzunguko wa pili kwa kuhakikisha kwamba inafanya vizuri katika michezo yote licha ya ushindani uliopo.

Akizungumzia kuanza kwa mzunguko huo wa pili hapo kesho, Hitimana amesema kuwa kama timu wamejipanga vizuri kutokana na michezo ya mwisho haikuwa na matokeo mazuri hivyo changamoto kubwa ilitokana na wachezaji wengi kuwa na majeraha lakini kwasasa wanne wamerejea jambo ambalo limeleta matumaini makubwa.

KMC kuikabili Coastal kesho

“Tunafahamu kuwa mzunguko wa pili utakuwa na ushindani zaidi kwani kila timu inahitaji kufanya vizuri na hivyo tunakwenda kupambana ili tupate matokeo mazuri kwa kuwa michezo yote ipo ndani ya uwezo wetu.

“KMC itawakosa wachezaji wawili ambao ni Hance Masoud na Emmanuel Mvuyekure kutokana na changamoto za majeraha huku wengine wakiwa kwenye ari na morali nzuri hivyo kila mmoja yupo tayari kutumika kwa ajili kupata alama.

Coastal Union ni timu nzuri hata ukiangalia katika mchezo wao wa mwisho walipata ushindi wakiwa ugenini, lakini hatuliangalii hilo kama changamoto badala yake tunajiandaa kwa ajili kuhakikisha kuwa tunatumia vizuri uwanja wetu wa nyumbani hapo kesho.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa