Ligi ya NBC kurejea hii leo baada ya kusimama kwa siku kadhaa kupisha michuano ya Mapinduzi Cup ambayo yanatamatika hii leo. Klabu ya KMC leo itakuwa mgeni wa Mtibwa Sugar.

 

KMC Ugenini Leo Dhidi ya Mtibwa Sugar

Mchezo huo wa KMC utapigwa katika uwanja wa Manungu mkoani Morogoro huku kila timu ikitafuta pointi 3 muhimu ili kuendelea kujiweka kwenye nafasi nzuri ya msimamo kabla ya ligi kufikia tamati.

Mtibwa Sugar na KMC wote wametoka kupoteza mechi zao mbili za mwisho, lakini Walima Miwa wana mechi 6 hawajapata ushindi wakienda sare mara tatu na kupoteza mara tatu.

KMC Ugenini Leo Dhidi ya Mtibwa Sugar

Wakati Wanakino Boys wao katika mechi zao sita za mwisho wameshinda mbili, sare mbili na kupoteza mara mbili, huku mechi ya mwisho kukutana timu hizi mbili vijana wa Thierry Hitimana waliibuka wababe.

Je hii leo inaweza kuwa ni nafasi kwa Mtibwa kulipiza kisasi kwa vijana wa Kinondoni ambao walichukua pointi zote sita msimu uliopita wakianza na leo wakiwa nyumbani?.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa