KLABU ya watoza Ushuru wa Kinondoni KMC FC wameapa kuharibu rekodi ya kutokufungwa kwa timu ya Yanga SC kwenye Ligi kuu Tanzania bara, ambapo klabu hiyo ya YANGA mpaka sasa ina jumla ya Michezo 43 ya Ligi kuu hawajafungwa huku wakiwa wamefungwa na AL Hilal mechi moja na kutoa sare mechi moja.

Mchezo huo utapigwa kwenye dimba la Benjamini Mkapa siku ya Jumatano tarehe 26/10/2022, ambapo Kino Boys atakuwa ugenini.

Kupitia ukurasa wao wa Twitter klabu ya Kino Boys imechapisha picha ikionesha hali ya kujiamini kwao, kuelekea mchezo huo ambao endapo wakishinda basi moja kwa moja wataongoza kwenye msimamo wa Ligi kuu hiyo ni kutokana na wao kuwa nafasi ya 3.

Mchezo wa mwisho wa Ligi Kino Boys walishinda dhidi ya Azam FC kwa mabao 2-1, na kuwafanya kuwa na uhakika wa nafasi nne za juu kwenye msimamo.56



JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa