KLABU ya KMC ambayo inadhaminiwa na kampuni bora ya ubashiri Tanzania ya Meridian Bet jana imepata ushindi wa kwanza ndani ya Ligi Kuu Bara baada ya dakika 90 kwenye Uwanja wa Uhuru kwa kuwalaza Ihefu Sc 2-1.

 

KMC Wameanza Kazi Ligi Kuu

Ni mshambuliaji mzawa, Matheo Anthony alipachika bao la mapema dakika ya 3 huku Raphael Daud dakika ya 34 aliweka usawa kwa Ihefu na kuwafanya waende mapumziko wakiwa wametoshana nguvu.


Kipindi cha pili KMC walianza kwa kasi kuliandama lango la Ihefu na walipata bao la ushindi dakika ya 77 kupitia kwa Nzigamasabo Styve.

 

KMC Wameanza Kazi Ligi Kuu

KMC inafikisha pointi tano ikiwa nafasi ya 8 huku Ihefu ambayo ipo chini ya Kocha Mkuu, Juma Mwambusi imegotea nafasi ya 16 ikiwa haijakusanya pointi.

Kwa msimu wa 2022/23 Kino Boys imepata ushindi wake kwa mara ya kwanza huku Ihefu ikiwa bado haijapata kushinda.

 

KMC Wameanza Kazi Ligi Kuu


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa