UONGOZI wa KMC umefunguka kuwa licha ya kiwango walichonacho Namungo lakini mipango yao kwenye mchezo huo ni kuhakikisha wanapata pointi tatu ambazo ni muhimu kwao.

Mchezo huo wa ligi kuu unatarajiwa kupigwa Oktoba mosi mwaka huu kwenye Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa, Lindi.

 

KMC Wanazitaka Tatu za Namungo

Akizungumzia maandalizi yao, Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema kuwa wanatambua ugumu wa mchezo huo lakini wamejipanga kwa ajili ya kuhakikisha wanapata pointi tatu.

“Kikosi chetu kinaendelea na mazoezi ya kujiandaa na mchezo ujao wa ligi dhidi ya Namungo na wachezaji wote wapo fiti na morali ipo juu.

 

KMC

 

“Tunajua hali ya Namungo ilivyo kwa sasa hivyo mchezo utakuwa wa ushindani mkubwa lakini kwa upande wetu tunahitaji pointi tatu ambazo zitakuwa muhimu sana kwa upande wetu.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa