Klabu ya KMC imeangukia pua leo katika mchezo wa ligi kuu ya NBC baada ya kukubali kichapo cha bao moja kwa sifuri dhidi ya mabingwa watetezi wa kombe hilo klabu ya Yanga.

KMC wamepoteza wa pili mfululizo baada ya kupoteza dhidi mchezo uliopita dhidi ya Ruvu Shooting leo tena wamekubali kichapo cha goli moja kwa bila dhidi ya Yanga, Kutokana kichapo hicho inawafanya vijana wa Kinondoni kua kwenye wakati mgumu kwani kwasasa wanakaribiana na vilabu ambavu vitacheza nafasi ya mtoano ili kubaki ligi kuu.kmcKlabu ya KMC kwasasa wana alama 23 baada ya kucheza michezo 23 ya ligi kuu ya NBC ikiwa ni wastani wa alama moja katika kila mchezo ambao wameucheza msimu huu, Hivo klabu hiyo inahitaji kupambana zaidi katika michezo yao inayofuata kwani hali imeanza kutokua shwari kwa upande wao.

Klabu ya Yanga leo ambao wamefanikiwa kupata alama tatu goli pekee likiwekwa kimiani na mshambuliaji kijana Clement Mzize wameweza kuendelea kujishindilia kieleni mwa msimamo wa ligi kuu ya NBC baada ya kufikisha jumla ya alama 62, Huku wakiwaacha watani zao kwa jumla ya alama 8.kmcKlabu ya yanga baada ya ushindi dhidi ya KMC leo wameweza kujitengenezea mazingira mazuri ya kutetea ubingwa wo ambao walitwaa msimu uliomalizika, Mpaka sasa klabu ya Yanga imebakiza michezo tisa sawa na wapinzani wao klabu ya Simba lakini wao wana faida ya alama 8 ambazo wamewaacha nazo wapinzani wao.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa