Baada ya kupata pointi tatu dhidi ya Tanzania Prisons, Kocha Mkuu wa kikosi cha Coastal Union, Yusuf Chipo amefunguka kuwa anazitaka pointi nyingine tatu mbele ya Mbeya City.

Coastal walipata ushindi huo jana alhamis kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya baada ya kuifunga Prisons kwa mabao 2-0.

Coastal Union, Kocha Coastal Union Anogewa na Ushindi, Meridianbet

Akizungumza baada ya mchezo huo, Chipo alisema: “Tunashukuru ushindi umepatikana leo kwenye Uwanja wa ugenini.

“Prisons ni timu nzuri ina wachezaji wazuri lakini sisi tulisoma mchezo hivyo walivyoanza kupiga mipira mirefu ilikuwa faida kwetu na kupata matokeo.

“Ni kweli mchezo ujao tutakuwa ugenini tena dhidi ya Mbeya City lakini tunaenda kuweka mikakati mipya kwa ajili ya kuhakikisha tunapata matokeo tena.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa