Kocha mkuu wa Simba Roberto Oliveira amerejea nchini kwao Brazil usiku wa jana kwa shughuli binafsi za kifamilia na anatarajia kurejea mwishoni mw amwezi huu wa Januari.

 

Kocha Mkuu wa Simba Roberto Oliveira Arejea Kwao Brazil

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 62, ameondoka klabuni hapo kwenda Brazil akiwa na siku 21 tuu toka ajiunge na Wekundu hao akitokea Vipers ya Uganda baada ya kutambulishwa rasmi Januari 3 2023.

Roberto toka ajiunge na Simba amesimamia mechi mbili mpaka sasa na kwenye hizo mechi ameshinda zote moja akiwa Benjamin Mkapa na nyingine akiwa ugenini huko Dodoma.

Kocha Mkuu wa Simba Roberto Oliveira Arejea Kwao Brazil

Kwenye mechi hizo mbili timu imeruhusu mabao mawili huku wakifunga mabao manne na pia kabla ya kuanza michuano ya Klabu Bingwa Afrika atacheza mchezo wa Ligi dhidi ya Singida Big Stars Februari 03.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa