Kocha Mpya Simba Anaitaka Nusu Fainali Afrika

Kocha mpya wa klabu ya Simba Roberto Oliviera ambaye ametambulishwa siku ya leo ndani ya klabu hiyo amesema mipango ya klabu hiyo ni kuifikisha timu hiyo hatua ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa Afrika.

Kocha huyo wa zamani wa Vipers ya Uganda ametambulishwa ndani ya timu hiyo mapema leo baada ya kutangaza kuondoka kwenye klabu ya Vipers siku kadhaa nyuma. Na moja ya mipango ya mwalimu huyo ni kuifikisha klabu ya Simba nusu fainali au fainali kabisa ya ligi ya mabingwa Afrika.kochaKlabu ya Simba imefanikiwa kufanya vizuri kwa muda mrefu kwenye ligi ya mabingwa Afrika na kufanikiwa kufika hatua ya robo fainali mara kadhaa, Hivo kufika hatua ya nusu fainali ni miongoni mwa mipango mikubwa ya klabu hiyo.

Kocha Roberto Oliviera amefanikiwa kufanya vizuri na klabu ya Vipers ambapo amefanikiwa kuiwezesha klabu hiyo kubeba taji la ligi kuu nchini Uganda, Kombe la Fa nchini humo, Pamoja na kuiwezesha klabu hiyo kufuzu hatua ya makundi ya ligi ya mabingw barani Afrika kwa mara ya kwanza.kochaViongozi wa klabu ya Simba wana imani kubwa na kocha huyo raia wa Brazil na wameweka matumaini yao kwa kocha huyo kuiwezesha tiimu hiyo kutimiza malengo yao ya muda mrefu kufuzu hatua ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa Afrika, Kuhusu kocha wasasa wa Simba Juma Mgunda bado klabu hiyo haijatoa taarifa rasmi kuhusu majukumu mapya ya mwalimu huyo.

Acha ujumbe