KOCHA MPYA SIMBA HUYU HAPA

SIMBA licha ya kuwa na mwenendo mzuri chini ya Kocha wa muda wa Sasa Juma Ramadhan Mgunda, bado inatajwa kuwa kwenye mipango ya kusaka mrithi wa Abdelhack BENCHIKA.

Yapo majina ya makocha kadhaa kutoka ndani na nje ya Afrika ambao wanatajwa kuja kuchukua nafasi ikiwemo pia jina la kocha wa Klabu ya FC San Pedro ya Ivory Coast, Muivory Coast Maxime Gouamene.Simba wanamtolea macho Gouamene kutokana na Mwendo mzuri akiwa na San Pedro, kwani anaongoza Ligi Kuu ya Ivory Coast akiwa na alama 48.

Maxime Gouamene pia alishaifundisha timu ya taifa ya ya Ivory Coast kwenye mashindano ya CHAN 2020, lakini pia alishawahi kuwa kocha msaidizi wa Ivory Coast kwenye Senior Team.simba, Ahmed AllyLakini pia nimemtafuta Zambro Traore ambae ni Agent ameniambia Maxime Gouamene ni moja ya kocha mzuri pale Ivory Coast.

Acha ujumbe