Baada ya kufanya mazoezi na kikosi cha Simba SC kwa siku tatu katika kambi nchini Dubai Kocha Mkuu Oliveira Roberto ‘Robertinho’ amejiridhisha kuwa anahitaji mshambuliaji mwingine ambaye ni hatari. Pata Odds kubwa za soka ukiwa na Meridianbet.
Robertinho amesema kikosi chake kina washambuliaji wazuri huku akimwagia sifa Nahodha John Bocco lakini ameweka wazi kuwa ili atimize malengo yake anahitaji mshambuliaji mwingine wa kusaidiana na waliopo.
“Aina ya mshambuliaji ninayemtaka ni mwenye nguvu, kasi na maarifa ya kufunga,” Robertinho.
Kikosi cha Simba SC kikiendelea na mazoezi mjini Dubai ambapo jana walifanya mazoezi mara moja na kuanzia jana timu itafanya mazoezi mara mbili yaani asubuhi na jioni. Ukiwa na meridianbet unaweza kubashiri mubashara, tembelea maduka ya meridianbet uweze kubashiri.
Kocha Robertinho anasema ameamua kuongeza muda wa mazoezi ili kupandisha nguvu ya timu (Intensity) pamoja na utimamu wa mwili (Body Fitness). Pata Odds kubwa za soka ukiwa na Meridianbet.
Simba SC inatarajia kucheza michezo miwili ya kirafiki kujipima nguvu kabla ya kurejea nchini, mchezo wa kwanza utapigwa Januari 13 dhidi ya Al Dhafra FC, kabla ya kukutana na CSK Moscow ya Urusi Januari 15, 2023. Meridianbet wanatoa ODDS kubwa kwenye mechi zote. Bashiri hapa.