Kaimu kocha Mkuu wa Namungo, Denis Kitambi amefunguka kilichomfelisha kupata matokeo kwenye mchezo wa jana dhidi ya Yanga ni makosa ya mabeki wake.
Namungo walipoteza mchezo wa ligi kuu jana jumatano kwenye Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa kwa mabao 2-0 yakifungwa na Yannick Bangala na Tuisila Kisinda.
Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Kitambi alisema “Kilichotukwamisha ni kukosekana kwa umakini kwenye eneo letu la ulinzi hasa mabeki wa pembeni.
“Mpango wetu wa kwanza ambao tulikuwa nao ulifeli kwani tulishindwa kuweka presha kubwa kwenye mpira hivyo hata ule tuliokuwa nao kwenye karatasi tulishindwa kuufanyia kazi.”