Kocha Pan Aitangazia Vita JKT

Kocha Msaidizi wa Pan African, Daudi Macha amesema kuwa mipango yao ni kupata ushindi kwenye mchezo wao wa ligi ya Championship dhidi ya JKT Tanzania.

Mchezo huo wa ligi utapigwa kesho jumapili kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar ambapo Pan watakuwa kwenye Uwanja wa nyumbani.

Pan African

Pan African wanaingia kwenye mchezo huo wakiwa na kumbukumbu ya kupata ushindi mnono wa mabao 3-1 dhidi ya Gwambina huku JKT Tanzania akiambulia suluhu mbele ya Green Warriors.

Akizungumzia maandalizi yao kuelekea kwenye mchezo huo, Macha amesema: “Maandalizi yamekamilika kuelekea kwenye mchezo huo kama tulivyopanga.

“Morali ipo juu kila mchezaji anahitaji kuipambania nembo ya timu kwa ajili ya kupata ushindi kwenye mchezo huo japo utakuwa mgumu.

“Mipango yetu kwenye mchezo wa kesho ni kuhakikisha tunapata ushindi mwingine ili tuweze kuendeleza rekodi ya ushindi hivyo JKT wajiandae kesho.”

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.