Kocha Pan Anazitaka Tatu za Mbuni

KIKOSI cha Pan African kimeanza mazoezi rasmi leo jumanne kwa ajili ya kujiandaa na mchezo ujao wa ligi ya Championship dhidi ya Mbuni FC huku Kocha Mkuu, Twaha Beimbaya akisema anahitaji ushindi kwenye mchezo huo.

Akizungumzia maandalizi yao, Beimbaya amesema kuwa “Wachezaji wote wameenea kikosini na leo tumeanza kufanya mazoezi ya utimamu kwa ajili ya kujiweka fiti.

 

Pan

“Tuna mchezaji mwenye majeraha mmoja tu ambaye ni Hassan Njete yeye aliumia kwenye mchezo uliopita dhidi ya Mashujaa ila anaendelea vizuri.

“Tulikosa pointi tano tukiwa ugenini baada ya michezo miwili hivyo tunajiandaa kuelekea mchezo ujao ambao tutacheza nyumbani dhidi ya Mbuni na tunahitaji ushindi kwenye mchezo huo.”

 

PAN

Pan African watashuka tena dimbani Oktoba 2, mwaka huu kumenyana na Mbuni kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar.

Acha ujumbe