Kocha Mkuu wa Simba, Fadlu Davies ameandaa sapraizi katika kikosi chake kabla ya kuivaa Yanga Alhamisi, Agosti 8, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa. Jisajili hapa kuwa wa kwanza kushinda Mamilioni ya Meridianbet kila siku.
Fadlu alitoa mapumziko kwa kikosi hicho huku akiwasihi wachezaji kuangalia mechi ya Yanga dhidi ya Red Arrows iliyopigwa juzi kwenye uwanja wa Mkapa katika kilele cha Wiki ya Wananchi.
Fadlu aliwasisitiza wachezaji kuiangalia vyema Yanga kwani ndiye mpinzani watakayekutana naye katika mchezo ujao wa nusu fainali ya Ngao ja Jamii kesho kutwa Alhamisi.
Beti na Meridianbet kwa ushindi mkubwa na odds kubwa, Ligi zinakaribia kuanza, usije kupishana na gari la Mshahara.
Wachezaji wa Simba wote walifanya hivyo ambapo baadhi yao walijumuika kwa makundi hususani wale wapya na kutazama mechi kwa pamoja katika hotel moja jijini Dar es Salaam huku wengine wakitazama wakiwa majumbani.
“Tuliambiwa kuangalia mechi, wapo waliokuwa hotelini kwa pamoja lakini wengine tulikuwa majumbani,” amesema mmoja wa wachezaji wa Simba na kuongeza;
“Hadi tunamaliza mechi yetu ya mwisho hakuna mchezaji aliyekuwa na uhakika wa nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza. Kocha huyu anapenda kila mtu acheze na ana uamuzi mgumu hivyo hadi sasa ukiniambia nikupangie kikosi cha kwanza siwezi.”
Wakati wachezaji wakiitazama mechi ya Yanga kwa namna tofauti, kocha Fadlu na benchi lake zima la ufundi nao waliitazama mechi hiyo kwa pamoja kiufundi zaidi.
Afisa habari wa Simba, Ahmed Ally alisema wameridhishwa na uwezo wa kikosi chao kipya na sasa wako tayari kuanza mapambano bila kuihofia timu yoyote.
“Tumekamilika na tumeridhika na timu yetu iliyosheheni vijana. Tupo tayari kwa mapambano na hili litathibitishwa Agosti nane tutakapocheza na Yanga, mtaona wenyewe namna timu ya kisasa inavyocheza,” alisema Ahmed.
Simba ilirejea mazoezini juzi Jumatatu, na leo itaendelea na programu ya mazoezi katika uwanja wake wa Mo Simba Arena uliopo Bunju Dar es Salaam.
Michezo ya Kasino na Sloti ni machimbo yanayotoa pesa kirahisi. Cheza kasino hapa.
This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.
Strictly Necessary Cookies
Strictly Necessary Cookie should be enabled at all times so that we can save your preferences for cookie settings.
If you disable this cookie, we will not be able to save your preferences. This means that every time you visit this website you will need to enable or disable cookies again.