Kocha Mkuu wa kikosi cha Simba Queens, Charles Lukula ameahidi kuwa anaenda kwenye michuano ya Ligi ya mabingwa Afrika kushindana na sio kushiriki.

Lukula amesema Licha ya kuwa na muda mchache tangu aanze kukinoa kikosi hicho lakini kila kitu kipo sawa kwa ajili ya kuhakikisha wanatimiza malengo yao.

Simba Queens, Kocha Simba Queens Aahidi Jambo, Meridianbet

“Tunaingia kwenye hayo mashindano tukiwa kama vibonde kwani ni mara yetu ya kwanza tunaenda kushiriki lakini tumejiandaa ili kuhakikisha tunafanya vizuri.

“Mipango yetu ni kuingia katika hatua ya nusu fainali na hilo linawezekana, kikosi ni kizuri na kipo fiti kwenda kupambana ili kutimiza malengo kwani hatuendi kushiriki tu bali kushindana.

“Nashukuru tangu nianze kukinoa kikosi hiki nimepata ushirikiano wa kutosha, tunajua tumebeba bendera ya Tanzania hivyo tutaenda kuwakilisha vyema taifa.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa