Kocha Mkuu wa Yanga, Miloud Hamdi ameweka wazi kuwa kwa wanaomtambua yeye ana uchu wa ushindi kwenye kila mechi ambazo wacheza ndani ya uwanja.

Baada ya kubeba mikoba ya Sead Ramovic amekiongoza kikosi cha Yanga kwenye mechi mbili dhidi ya JKT Tanzania na KMC,kwenye msako wa pointi sita ni nne kaambulia kwa ushindi mchezo mmoja na kugawana pointi mojamoja mbele ya JKT Tanzania.
Kocha huyo Februari 17 ana kibarua cha kuiongoza timu hiyo kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Singida Black Stars unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa KMC, Complex.
Miloud amesema: “Wanaonifahamu wanajua namna gani nina kuwa na uchu wa kupata ushindi, lakini hilo haliondoi ukweli kwamba tunapaswa kuwaheshimu wapinzani ambao tunakutana nao uwanjani, kikubwa ni umakini na kutumia vema nafasi ambazo tunazipata uwanjani.



