USHINDI wa bao 1-0 lililofungwa na Azizi Ki kwenye mchezo wa marudiano Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Club Africain ya Tunisia, umemuibua Kocha Msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze ambaye amechimba mkwara mzito akisema sasa wanashusha balaa hilo kwenye mashindano ya ndani kwa lengo moja tu, la kuhakikisha wanashinda michezo yao na kutetetea ubingwa wa ligi kuu na Kombe la Shirikisho Afrika

Yanga juzi Jumatano waliandika rekodi mpya katika mashindano ya kimataifa mara baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Club Africain katika mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika.kazeMabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara wanaongoza msimamo wa ligi na pointi zao 20 walizokusanya katika michezo nane waliyoicheza, wanatarajia kurejea nchini leo wakitokea Tunisia tayari kwa ajili ya ratiba ya michezo yao inayofuata ya Ligi Kuu Bara.

Kaze alisema: “Haikuwa kazi rahisi kwetu kufanikisha hili, wachezaji wetu wanastahili pongezi kubwa kwa kupambana kwa dakika zote 180 za michezo hii miwili na nadhani sasa tunarudi nyumbani kujipanga na michezo yetu ijayo.

“Lakini naweza kusema hizi ni kama salamu sasa kuwa tunarejea nyumbani kama mabingwa kuhakikisha tunashinda tena taji la Ligi Kuu Bara na lile la Kombe la Shirikisho la Azam.”

aviator

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa