KONKONI AKANUSHA KUONDOKA YANGA

BAADA ya kusambaa kwa taarifa kuwa Hafiz Konkoni anaenda kwao Ghana kwa mkopo, mshambuliaji huyo amekanusha taarifa hizo na kusema kuwa haondoki Yanga na atakuwa sehemu ya timu hiyo hadi mwisho wa msimu.

Konkoni alijiunga na Yanga mwishoni wa dirisha la usajili la mwaka jana na tangu amejiunga na klabu hiyo amekuwa hapati nafasi ya kucheza mara kwa mara.KONKONIAkizungumzia uvumi wa kuwa anataka kuondoka Yanga alisema: “Mimi nimeomba tu ruhusa kwa kocha na nikapewa ruhusa ya kuondoka ili niweze kutatua masuala ya familia yangu, nimeomba tu ruhusa nirudi Dar es Salam ili niweze kutatua masuala ya kifamilia nikiwa Dar Es Salaam.

“Siendi Ghana, nimekuja Dar es Salam ili nitume pesa nyumbani, Kwa sababu nikiwa Zanzibar nimeshindwa kufanya uhamisho wa fedha kwenda nyumbani.

“Lakini nimeshangazwa na hizi taarifa kama naondoka kwenda Ghana kwa ajili ya usajili wa mkopo jambo ambalo sio kweli, na tayari nipo Dar Es Salam.

Acha ujumbe