Konkoni wa Yanga Anaitaka Ligi Kuu

MSHAMBULIAJI mpya wa Yanga, Mghana, Hafiz Konkoni amebainisha kwamba, ana furaha kujiunga na timu hiyo, huku akisema ana deni kubwa la kulilipa ambalo ni kutetea makombe yote yaliyobebwa na Yanga msimu wa 2022/23.

Kauli ya mshambuliaji huyo huenda ikawa salamu kwa Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally ambaye ametamba kuwapoka Yanga makombe wanayoyatetea, ambayo Simba imeyakosa kwa misimu miwili mfululizo.YangaMghana huyo tayari ameripoti kambini Kijiji cha Avic Town, Kigamboni nje kidogo ya Dar, kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao mara baada ya kutambulishwa klabuni hapo akitokea Bechem United ya Ghana.

Kwa mujibu wa mshambuliaji huyo, kikubwa alichopanga ni kuifanyia timu hiyo makubwa kama ilivyokuwa msimu uliopita ikiwemo kutetea makombe waliyobeba ambayo ni Ngao ya Jamii, Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho la Azam Sports.

Konkoni alisema, kingine kikubwa atakachokifanya ni kuhakikisha anaifikisha Yanga katika nafasi nzuri ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya msimu uliopita kufanikiwa kucheza Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Aliongeza kuwa, kama mchezaji, atatimiza majukumu yake ya uwanjani ikiwemo kufunga na kutengeneza nafasi kwa wenzake huku akikataa kufananishwa na mshambuliaji aliyepita, Fiston Mayele.

“Ni furaha kubwa kujiunga na klabu hii kubwa ya Yanga, yenye historia kubwa zaidi katika Bara la Afrika. Niahidi kufanya kazi kwa bidii kwa lengo la kuitangaza.Yanga“Nina furaha kuwepo hapa Yanga, timu yenye mashabiki wa ajabu ambao katika historia yangu ya soka sijawahi kuwaona wa aina hii, kikukweli ninawapenda wote na ninaahidi kufanya kila ninaloliweza kwa ajili ya klabu wakati wowote.

“Nimekuja mwenyewe Yanga kwa mapenzi yangu, na mara baada ya kupata taarifa za mimi kuhitajika, sikusita na haraka nikakubali kuja kujiunga nayo kwa ajili ya msimu ujao ambao ninakwenda kuifanyia mengi makubwa timu yangu mpya,” alisema Konkoni.

Acha ujumbe