KRAMO AREJEA MAZOEZINI SIMBA

WINGA wa Simba Aubin Kramo ameanza mazoezi katika viwanja vya MO Simba Arena.

Raia huyo wa Ivory Coast aliyeibuka ndani ya Simba akitokea ASEC Mimosas hakuwa fiti Jambo lililomuweka nje ya uwanja.

Kramo aliumia kwenye mazoezi ya kujiandaa na mechi za Ngao ya Jamii kule Tanga, Uwanja wa Mkwakwani.KRAMOSimba ilicheza mechi mbili dhidi ya Singida Fountain Gate hatua ya nusu fainali ya pili na ule wa fainali dhidi ya Yanga.

Kwenye mechi zote hizo mbili Simba haikufunga mabao ndani ya dakika 90 iliambulia ushindi kwa penalti hata ilipocheza fainali na Yanga.
Daktari wa Simba, Edwin Kagabo alibainisha kuwa nyota Aubin Kramo  alipata maumivu kwenye mguu jambo lililofanya asionekane uwanjani.KRAMO“Maendeleo yake ni mazuri na atarejea uwanjani hivi karibuni baada ya kupata matibabu,”

 

Acha ujumbe