Ligi Kuu Kinawaka Mapema Tu

LEO Agosti 7 Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) kupitia Afisa Mtendaji Mkuu, Almasi Kasongo, imetangaza ratiba ya msimu mpya wa 2023/24.

Katika ratiba hiyo inayotarajiwa kuanza Agosti 15 2023 mchezo wa kwanza wa kufungua pazia utachezwa Uwanja wa Highland Estate, Mbeya.
Ihefu wao watakuwa nyumbani wakiikaribisha Geita Gold inayonolewa na Kocha Mkuu, Hemed Morocco.ligi kuuKasongo amesema mechi ya watani wa jadi kati ya Simba SC dhidi ya Yanga SC itapigwa Novemba 5, 2023 saa 11:00 jioni katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Katika mechi za mzunguko wa kwanza kwenye msimu mpya wa NBC Premier League 2023/24, Simba mchezo wake wa kwanza itakuwa ugenini dhidi ya Mtibwa Sugar.

Mchezo wa Simba inayonolewa na Kocha Mkuu Roberto Oliveira unatarajiwa kuchezwa Agosti 17,2023 Uwanja wa Manungu, Morogoro.ligi kuuYanga SC inayonolewa na Kocha Mkuu Miguel Gamondi itaanza nyumbani dhidi ya KMC mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
Burudani ya kwanza kwa Yanga inatarajiwa kuchezwa Agosti 23,2023 ambapo timu hizo zitakuwa kusaka pointi tatu muhimu.

Ipo wazi kuwa mabingwa watetezi wa ligi ni Yanga waliotwaa ubingwa huo chini ya Nasreddine Nabi.

Acha ujumbe