Mjumbe wa Bodi wa klabu ya Simba, Mohamed Dewji amefunguka na kusema kuwa, kipa namba moja wa Simba, Aishi Manula ni kipa bora Afrika.

Dewji aliyasema hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram na kuandika kuwa: “Lazima nikiri kwamba Manula ni moja wa makipa bora barani Afrika.”

DEWJI, DEWJI: Manula Ndio Kipa Bora Afrika, Meridianbet

Maneno hayo yaliambatana na video ikimuonyesha Manula akiokoa hatari langoni mwake katika mchezo wa marudiano dhidi ya Nyasa Big Bullets uliochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa wikiendi iliyopita.

Kwenye mchezo huo wa mtoano kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika Simba aliibuka na ushindi wa mabao 2-0 na kufanikiwa kutinga raundi ya kwanza ikitarajiwa kucheza dhidi ya Clube Desportivo 1 de Agosto kutoka Angola.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa