FEISAL SALUM ANAFUNGA NA KUWATESA YANGA

WAKATI Azam FC inakomba pointi tatu dhidi ya JKT Tanzania Jana kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Meja Isamuhyo, Feisal Salum kiungo mshambuliaji wa Azam FC aliendelea kuwasha moto kama kawaida.

Katika dakika 90 alizocheza na kushuhudia ubao ukisoma JKT Tanzania 0-2 Azam FC, yeye akifunga bao Moja na alipiga mashuti matatu ambayo yalilenga lango na katika hayo moja lilizama nyavuni akitumia mguu wake wa kulia.feisal salumFeisal Salum alipachika bao lake la 16 dakika ya 90+4 na bao la kwanza lilipachikwa na Abdul Sopu dakika ya 30 kipindi cha kwanza cha mchezo huo.

Matokeo hayo yanaifanya Azam FC kubaki namba mbili na pointi 63 baada ya kucheza jumla ya mechi 28 wapo sawa na Simba iliyo nafasi ya tatu tofauti kwenye mabao ya kufungwa.

Azam FC imefungwa mabao 20 huku ukuta wa Simba ukiwa umeruhusu kufungwa mabao 25 kwenye mechi 28.

Feisal Salum anafikisha mabao 16 akiwa namba moja kwa vinara wa utupiaji Bongo huku akiwa katoa jumla ya pasi 7 za mabao msimu wa 2023/24.feisal salumHuku Yanga kichwa kikiwauma kwenye vita ya Ufungaji Bora kwani Moja ya kitu ambacho hawapendi kitokee ni Feisal kuwa mfungaji Bora Msimu huu.

Acha ujumbe