BAADA ya kumalizika kwa mizunguko miwili ya ligi kuu Bara, golikipa wa Simba, Aishi Manula ameibuka kinara wa Clean Sheet kutokana na kutoruhusu bao lolote.

Timu ya Simba chini ya Kocha Mkuu, Zoran Maki imeshinda mechi zote mbili kwa jumla ya mabao matano huku wakiwa hawajaruhusu bao lolote.

Manula anaibuka na rekodi hiyo katika michezo hiyo miwili waliyocheza Simba dhidi ya Geita Gold (3-0) na Kagera Sugar (2-0).

Makipa wengine ambao wana clean sheets moja ni Metacha Mnata (Singida Big Stars), Mahamoud Humid (Coastal Union), Hussein Masalanga (Ruvu Shooting), Jonathan Nahimana (Namungo) na Abutwalib Mshery (Yanga).

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa