Olise Atwaa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ufaransa Anayecheza Nje ya Nchi

Kiungo mshambuliaji wa Michael Olise ameendelea kuthibitisha ubora wake baada ya kutwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Ufaransa Anayecheza Nje ya nchi, akiwapiku mastaa wengine wakubwa akiwemo Kylian Mbappe pamoja na Rayan Cherki.

Olise Atwaa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ufaransa Anayecheza Nje ya Nchi

Olise ameonyesha kiwango cha hali ya juu katika msimu huu kupitia mchango wake mkubwa ndani ya kikosi chake, ambapo amehusika moja kwa moja katika mabao 52 ndani ya michezo 50 aliyocheza kwenye mashindano mbalimbali. Takwimu hizo zimezidi kuwavutia wadau wengi wa soka barani Ulaya.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Katika mafanikio hayo, nyota huyo amefunga mabao 20 huku akitoa pasi 30 za mwisho zilizozaa mabao, jambo lililoonyesha uwezo wake mkubwa wa kutengeneza nafasi na kuiongoza safu ya ushambuliaji kwa ubunifu mkubwa uwanjani.

Olise Atwaa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ufaransa Anayecheza Nje ya NchiAkizungumzia mafanikio hayo, Olise alieleza kufurahishwa na namna msimu wake ulivyokuwa mzuri huku akisisitiza kuwa mafanikio hayo yametokana na ushirikiano mkubwa kutoka kwa wachezaji wenzake pamoja na benchi la ufundi. “Ninafurahia kutambuliwa kwa kazi yangu, lakini mafanikio haya ni matokeo ya juhudi za timu nzima,” alisema nyota huyo.

Olise Atwaa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ufaransa Anayecheza Nje ya NchiUbora wa Olise umeendelea kumuweka katika daraja la juu miongoni mwa wachezaji wa Kifaransa wanaocheza nje ya nchi yao, huku wachambuzi wengi wakimtaja kama mmoja wa mastaa wenye ushawishi mkubwa katika soka la Ulaya kwa sasa kutokana na uwezo wake wa ubunifu na mchango mkubwa kwenye ushambuliaji.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.