WAKIJIANDAA na mchezo wa pili wa ligi dhidi ya Mashujaa, kikosi cha Pan African kinatarajia kujipima nguvu na Rhino Rangers.

Mchezo huo wa kirafiki unatarajiwa kupigwa Septemba 21 mwaka huu kwenye Uwanja wa Vita, mkoani Tabora ambapo Pan wameweka kambi yao kujiandaa na mchezo wa ligi dhidi ya Mashujaa.

PAN, Pan Kujipima na Rhino Rangers, Meridianbet

 

Akizungumzia maandalizi ya mchezo wao dhidi ya Mashujaa, Ofisa Habari wa Pan African, Leen Essau amesema: “Wachezaji wote wapo sawa na wanaendelea na programu ya kocha kuelekea mchezo ujao.

“Tutacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Rhino Rangers Jumatano hii kwenye Uwanja wa vita hayo pia ni maandalizi ya kuwakabili Mashujaa kwenye mchezo ujao wa ligi.”

Pan African tayari wamecheza mechi moja ya ligi dhidi ya Kitayosce ambapo mchezo huo ulimalizika kwa sare ya bao 1-1.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa