Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara mara 28, Yanga wachezaji wao rasmi wameanza mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya katika Mji wa Avic Town, Kigamboni ilipo kambi yao.

Jana jioni ya Julai 23. Wachezaji wa kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi walianza mazoezi kwa ajili ya msimu mpya wa 2022/23.

Yanga, Yanga Wameanza Kazi Kigamboni, Meridianbet

Kambi yao haijachelewa kuanza kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli bali ni mpango kazi kutokana na wachezaji kupewa mapumziko.

Miongoni mwa mastaa ambao wameanza mazoezi ni pamoja na Denis Nkane, Aziz KI,Dickson Ambundo,Eric Johora pamoja na Yusuph Athuman.


 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa