Lomalisa Bado Yupo Sana Yanga

Lomalisa

BEKI wa kushoto wa Yanga, Joyce Lomalisa amekubali kubaki kuendelea kukipiga katika klabu hiyo hadi msimu ujao. Tembelea duka la ubashiri-Meridianbet kutandika jamvi lako kwa odds kubwa.

Hiyo ikiwa ni siku chache tangu beki huyo kipenzi cha Yanga kutishia kuondoka klabuni hapo na kwenda kutafuta changamoto sehemu nyingine.

Ukiwa na meridianbet odds kubwa, kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti.

Beki huyo alitishia kuandika barua ya kusitisha mkataba wake wa mwaka mmoja uliobaki huku akihusishwa kutakiwa Azam FC.

Beki huyo alikutana na viongozi wa timu hiyo, kwa ajili ya kufanya kikao kizito na kufikia muafaka wa kubakia hapo.

Beti na Meridianbet kwa odds kubwa na machaguo kibao, pia unaweza kubashiri mubashara.

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa, katika makubaliano hayo, beki ametoa sharti la kumalizia msimu wake wa mwisho kabla ya mazungumzo mengine kufanyika ya kubaki kukipiga hapo.

Aliongeza kuwa beki amekubali kutoa ushirikiano kwa benchi jipa la ufundi la timu hiyo, litakalokuwa chini ya Muargentina, Miguel Gamondi.

“Ishu ya Lomalisa na Yanga imemalizika baada ya viongozi kufanya naye kikao jana (Juni 27/2023) Jumatano na kufikia muafaka mzuri wa pande zote mbili za kubakia hapo.

“Hivyo katika kikao hicho Lomalisa amekubali kutoa ushirikiano mkubwa kwa benchi jipya la ufundi.

“Lomalisa ametoa ahadi ya kuipambania timu katika mashindano yote watakayocheza msimu ujao,” alisema mtoa taarifa huyo.

Lomalisa kupitia ukurasa wake wa kijamii alithibitisha kubakia Yanga kwa kusema kuwa: “Nipo tayari kuipambania Yanga katika msimu ujao.”

Odds kubwa kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti ni vitu vinavyoweza kubadilisha maisha yako kwa kukupatia pesa nyingi. Ingia mchezoni hapa.

Acha ujumbe