Lukelo Willilo Aula Afrika Zone 3 Ngumi za Ridhaa

Rais wa ZONE 3 Bw. Otieno Ombok “Jamal” amemteua Bw. Lukelo Willilo kutoka Tanzania kuwa Katibu Mkuu wa ZONE 3 kuanzia tarehe 11 Desemba, 2022 huko Abu Dhabi-UAE.

 

zone 3

Bw Willilo ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Ngumi Tanzania na mjumbe wa bodi ya AFBC atashirikiana na wajumbe wengine wawili Bw. Joseph Nkamicaniye kutoka Burundi na Abdulrahman Ali Mire kutoka Somalia.

Bw. Jamal pia alimteua Bw. Kalong Andre Basil ambaye ni Katibu Mkuu wa AFBC na aliyekuwa Katibu Mkuu wa ZONE 3 kuwa Mshauri wa KANDA YA 3.

Lakini pia imethibitishwa kuwa Mashindano ya Elite ZONE 3 yatafanyika kuanzia tarehe 16 – 22 Machi, 2023. Nchi mwenyeji itatangazwa baadaye.

ZONE 3 inajumuisha nchi 14 zifuatazo
1. Kenya 🇰🇪
2. Tanzania 🇹🇿
3. Uganda 🇺🇬
4. Burundi 🇧🇮
5. Somalia 🇸🇴
6. Ethiopia 🇪🇹
7. Kamerun 🇨🇲
8. Chad 🇹🇩
9. Jamhuri ya Afrika ya Kati 🇨🇫
10. Gabon 🇬🇦
11. DR Congo 🇨🇩
12. Kongo Brazzaville
13. Guinea ya Ikweta 🇬🇶
14. Rwanda 🇷🇼


Beti mechi zijazo za kombe la dunia na nyingine kupitia Meridianbet, beti na kitochi bila bando, kwenye machaguo spesho ya kombe la dunia yenye ODDS kubwa na bomba, na kama sio mpenzi wa mpira kuna michezo ya kasino mtandaoni napo unaweza kushinda jakipoti kubwa. Beti hapa.

Acha ujumbe