BAADA ya kufunga bao la tano kwenye ligi kuu kwa msimu huu, mshambuliaji wa Namungo, Relliants Lusajo amesema kuwa malengo yake ni kuwa mfungaji bora.

Lusajo anaongoza kwenye msimamo wa wafungaji mpaka sasa ambapo jana amefanikiwa kufunga bao pekee ambalo limeipa ushindi timu yake dhidi ya Coastal Union.

Akizungumzia mipango yake Lusajo amesema kuwa: “Najisikia furaha kufunga bao pekee ambalo limeipa ushindi timu yangu.


“Malengo niliyonayo kwa msimu huu kwanza ni kuisaidia timu yangu kutimiza malengo tuliyojiwekea lakini kwa upande wangu ni kufanikiwa kuwa mfungaji bora.”


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa