LYANGA AINGIA KWENYE RADA ZA YANGA

MKALI kutoka kwa matajiri wa Dar, Ayoub Lyanga anatajwa kuwa kwenye rada za mabosi wa mitaa ya Jangwani, Yanga kwa ajili ya kupata changamoto mpya.
Ipo wazi kuwa nyota huyo ambaye ameibukandani ya Azam FC akitokea Coastal Union alikuwa anapigiwa hesabu na mabosi hao kitambo.

Ni Yanga na Simba walikuwa wanahitaji saini ya Lyanga lakini Azam FC wakiamua jambo lao hawashindwi hivyo waliinasa saini ya nyota huyo ambaye ni winga.lyangaTetesi zinaeleza kua Ayoub Lyanga kwa sasa yupo kwenye mazungumzo ya mwisho na mabosi wa Azam FC ili kujadili kuongeza kandarasi mpya ama kumpa mkono wa asante.

Timu ambayo inamtazama winga huyo mwenye uwezo mkubwa kutumia mguu wake wa kushoto ni Yanga.

Acha ujumbe