Straika wa Azam FC, Abdul Sopu ameshauriwa na madaktari kupumzika kutokana na maumivu yanayomsumbua.

Sopu alijiunga na kikosi cha Azam msimu huu akitokea Coastal Union baada ya kuonyesha kiwango kizuri msimu uliopita.

Azam, Madaktari Wampumzisha Straika Azam, Meridianbet

Akizungumzia hilo, Kaimu Ofisa Habari wa Azam FC, Hasheem Ibwe amesema: “Kwa sasa kikosi kinaendelea vizuri na mazoezi kuelekea mchezo wetu dhidi ya Dodoma Jiji.

“Bado tutaendelea kumkosa beki wetu Malickou Ndoye ambaye anasumbuliwa na majeraha pamoja na Abdul Sopu.

“Sopu alifanyiwa vipimo akaonekana hana majeraha yeyote lakini baada ya kurejea mazoezini akasema bado anasikia maumivu hivyo madaktari wameshauri apumzike kwa muda kwanza ili baadae arejee kikosini.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa