Mamadou Doumbia ni Mali ya Yanga

Yanga hawajaishia kwa Metacha pekee, lakini pia wameleta beki mwingine Mamadou Doumbia ambaye atashirikiana na kina Bakari Mwamnyeto, Kibwana Shomari, Job katika eneo la ulinzi.

 

Mamadou Doumbia ni Mali ya Yanga

Mamadou anatokea Taifa la Mali na ana umri wa miaka 27 na anatokea katika timu ya Stade Malien ya huko Mali ambao ndio mabingwa wa Ligi hiyo.

Timu amabzo amecheza beki huyo ni pamoja na OC Safi, Stade Malien na ana mataji saba ya mashindano mablimbali ambayo amewahi kushiriki. Yanga wamemsajili mchezaji huyo maalumu kwaajili yaΒ  Kombe la Shirikisho lililopo mbele yao.

Mamadou Doumbia ni Mali ya Yanga

Hivyo mpaka sasa Yanga imemsajili kiungo mzawa Mudathir Yahaya, huku pia wakiwa wamemalizana na Kennedy Musonda ambaye amekuja kuchukua nafasi ya Heritier Makambo, ambaye ameondoka klabuni hapo.

Wakamalizia na Metacha Mnata pamoja na Mamadou Doumbia katika eneo la ulinzi, hivyo jumla ya wachezaji ni wanne katika Dirisha hili dogo.

 

 

Acha ujumbe