Msemaji na muhamasishaji wa klabu ya Yanga Haji Sunday Manara amerusha vijimbe kwa lugha ya picha baada ya kuzuiwa kujishughulisha na mchezo wa soka ndani na nje ya nchi kwa muda wa miaka miwili.

Manara na raisi wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF Wallace Karia kwenye mchezo wa fainali ya Azam Federation Cup kulitokea sintofahamu na wawili hao kurushiana maneno ambayo yalipelekea msemaji huyo kupelekwa kwenye kamati ya nidhamu.

Manara, Manara Atema Nyongo, Meridianbet

Kwenye ukurasa wake wa Instagram Manara aliandika: Kumbe Tatizo ni hili?
Uhhhh lalalaah Wamebugi kwangu Sitawaacha Wananchi, na litakuwa Tamasha kubwa kuliko walivyodhamiria.

“Simjui yoyote nchi hii anaenisogelea kwa kufuatiliwa ktk Instagram ,kwa Watu wa football na Sports kwa ujumla kunizidi, nguvu hyo niliojaaliwa na Mungu,ntaitumia effectively kulipush hili Concert kuu la kisoka. Ikiwa Parade yetu ilivunja Rekodi why tushindwe hili?

“Msifadhaike hata kidogo,,tuombe uhai tu coz dhulma huwa haina mwisho mwema na always haki hushinda,,ni suala la muda tu

“Sipoi hata tone na tabu ipo pale pale sanasana ndio itazidi,,otherwise waje kuniua, Yanga Bingwa na mm ndio Bugati”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa