Msemaji wa zamani wa Yanga Haji Manara ameibuka na kusema kuwa, kipa wa timu hiyo Djudjui Diarra yupo kwenye daraja la peke yake na siyo sawa kama utamlinganisha na makipa wengine wa ligi kuu.

Manara alikiri kuwa wapo makipa bora kwenye ligi kuu lakini linapokuja suala la Diarra na makipa hao inatakiwa yeye abaki kwenye daraja lake kutokana na ubora mkubwa anaonyesha akiwa langoni.

Manara, Manara: Diarra Yupo kwenye Daraja la Peke Yake, Meridianbet

Manara aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kuwa: “Ni kweli tuna makipa bora sana kwenye ligi kuu yetu ila kuwafananisha makipa wetu na Diarra ni kujitafutia dhambi kama za kuzini tu.

“Huyu hadaki tu kizamani kama watangazaji wetu wa wakati ule walivyokuwa wakitangaza, kadaka kama Nyani.

“Huyu ni kipa wa kisasa, anafanya saves ile kurukia mpira kama Nyani ni uzamani, kazi ya kipa wa kileo ni kuzuia lango lake mpira usingie, sio kuruka ruka hovyo.

“Kisha anawazidi wote chini, yeye ni ‘Sweeper’ kisha ‘ball control’ yake ni ya makipa wa hadhi ya kidunia,, anaanzisha mwenyewe mashambulizi, tena sio Kwa kurusha ili kuwahi counter attacks, anapasia kwa miguu yake.

“Kubwa ni Commanding Goalkeeper, ni kiongozi ndani ya uwanja. Kiukweli ubora wake ni mkubwa kuliko maradufu ya wenzake, kawaacha mbali mno. Yeye yupo Makka wenzake wapo Namtumbo.”

Diarra aliibuka shujaa kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Kagera ambapo aliokoa penalty iliyosababisha waondoke na alama tatu kwenye mchezo huo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa