MANULA: ASEC SIO WEPESI HATA KIDOGO

Kipa wa Simba Aishi Manula amesema mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ASEC Mimosas siyo rahisi wanapaswa kujiandaa sana.

Simba watakuwa na kibarua Cha kuwavaa Asec kesho Ijumaa nchini Ivory Coast.

Manula alisema mchezo utakuwa mgumu kwa sababu licha ya wapinzani wao kuwa wameshafuzu hatua ya mtoano, lakini bado wanahitaji matokeo ya ushindi ili waongoze kundi lao.manulaASEC Mimosas mpaka sasa wanaongoza kundi B wakiwa na Pointi 10, wakifuata Simba nafasi ya pili wenye pointi 5, Jwaneng Galaxy wana pointi 4 wakiwa nafasi ya tatu na nafasi ya nne ni Wydad AC wenye pointi 3.

Acha ujumbe