Ishu ya Manzoki na Simba imekaa hivi

KUELEKEA usajili wa dirisha dogo, Uongozi wa Simba umeweka wazi kuwa kocha mkuu wa kikosi hicho, Juma Mgunda, tayari amekutana na viongozi wa Bodi ya Wakurugenzi na kuwasilisha ripoti ya maboresho ya kikosi chake, huku jina la straika, Cesar Manzoki likijadiliwa kwa ukubwa.

Dirisha dogo la Usajili linatarajiwa kufunguliwa Desemba 16, mwaka huu na kufungwa Januari 15, 2023 ambapo timu za Ligi Kuu Bara, Championship na First League zinapata nafasi ya kufanya maboresho ya vikosi vyao.

Ishu ya Manzoki na Simba imekaa hivi

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, alisema: “Baada ya kufanya tathmini ya kikosi chake kupitia michezo 15 ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara, Kocha Mkuu Juma Mgunda wiki hii alikutana na uongozi wa juu wa timu na kuwasilisha ripoti ya usajili wa majembe mapya.

“Hatua inayoendelea hivi sasa ni viongozi wa Bodi kufanyia kazi mapendekezo hayo kabla ya kuandaa taarifa rasmi ambayo itakuja kwetu na kuiwasilisha kwa umma juu ya nani na nani anakuja Simba.

“Kuhusu Manzoki ni kweli kumekuwa na mawasiliano kati yetu na kama kila kitu kitaenda sawa, basi atakuwa miongoni mwa wachezaji wa Simba.”

Acha ujumbe