Mashabiki wa klabu ya Yanga wataingia bure katika mchezo wa ligi ya mabingwa Afrika hatua ya Robo Fainali dhidi ya klabu ya Mamelodi Sundowns utakaopigwa tarehe 30 mwezi huu.
Afisa Habari wa klabu ya Ali Kamwe wakati akizungumza na wanahabari leo kuelekea mchezo huo amesema mashabiki wa eneo la mzunguko wataingia bure katika katika mchezo huo dhidi ya Mamelodi.Mashabiki wa klabu ya Yanga watapata fursa ya kuingia bure katika mchezo huo na hii ni kutoa nafasi ya mashabiki wa klabu hiyo kupata nafasi ya kuingia uwanjani kwa wingi kuipa timu yao hamasa katika mchezo huo muhimu.
Msemaji Ali Kamwe amesema uongozi wa klabu yake hauna tamaa ya fedha na ndio maana wameamua kuondoa kiingilio kwenye eneo la mzunguko, Huku akidai wao wameweka maslahi ya mpira mbele kuliko fedha.Mashabiki wa klabu ya Yanga kwasasa wanachotakiwa kukifanya ni kujitokeza uwanjani kwa wingi kuipa sapoti timu katika mchezo huo muhimu kabisa dhidi ya Mamelodi Sundons kutoka Afrika ya Kusini.