Mashindano ya Ngumi za Ridhaa kwa Klabu Bingwa DSM 2022 (Club Championship DSM 2022) yanaanza rasmi leo jumatatu tarehe 21-11-2022 mpaka 24-11-2022 katika uwanja wa ndani wa Taifa wa Benjamin Mkapa, Dar es salaam.
Jumla ya wachezaji 94 kutoka katika vilabu 13 ikiwemo 1 kutoka Burundi vitashiriki mashindamo haya na leo Jumapili zoezi la uhakiki wa taarifa za wachezaji (Sports entry check) na upangaji wa ratiba umefanyika (Official Draw)
Mashindano haya yatafanyika kwa siku 4 na kesho siku ya ufunguzi kutakua na jumla ya mapambano 15 (Bouts)

Timu zinazoshiriki kwenye mashindano hayo ni MMJKT ambao ni mabingwa watetezi, Ngome JWTZ, Iringa Boxing Club, Kagera Boxing, Yombayomba Boxing Club, JKT Kibiti, JKT Mgulani, Urafiki Boxing Club, JKT Chang’ombe, Green Warriors, Dago Stars Boxing, Burundi Boxing na Band Coy.
Michezo hii itakua inafanyika kila siku kuanzia majira ya saa 9 alasiri.
Kombe la Dunia Linatimua Vumbi huko Qatar ni timu 32, sawa na mechi 64 zitapigwa kwenye viwanja tofauti. Meridianbet wana uwanja wao wa Kushiriki na wewe wakati Michuano hii inaendelea. Uwanja wa Machaguo Spesho ni Kwa ajili yako, wewe Bingwa wa Kubeti. Unaweza kubeti ni Timu gani itachukua Ubingwa, Timu gani Itaongoza kuwa na kadi nyingi za Njano na Nyekundu, au Timu gani itatoka mapema kwenye michuano hiyo. Uamuzi ni wako. Chaguo ni lako. Hii ipo mpaka mwisho wa Kombe la Dunia.