Mastaa 5 Yanga Mguu Ndani, Nje vs Mamelodi Sundowns Pacome Iko Hivi.

Zikiwa zimesalia siku 9 kuelekea mchezo wa kwanza wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga SC dhidi ya Mamelodi Sundowns kutoka Afrika ya Kusini, Ali Kamwe Afisa Habari wa Yanga Ali Shaban Kamwe ametoa taarifa ya majeruhi ya wachezaji klabu wanaofikia watano (5). Jisajili na Meridianbet upate bonasi za kasino kibao na odds kubwa za ubashiri kwa machaguo kibao.

Mamelodi Sundowns

 

Kamwe ametoa taarifa hiyo kwenye mkutano na waandishi wa Habari kuelekea mchezo huo utakaopigwa kwenye dimba la Mkapa majira ya Saa 3:00 Usiku, alisema kuwa mchezaji Kibwana Shomari amekwisha aanza kufanya mazoezi mepesi na wenzake hivyo uwezekano wa kucheza kwenye mchezo huo ipo endapo mwalimu atapanga kumtimua. Beti na Meridianbet kwa odds kubwa na machaguo kibao, pia unaweza kubashiri mubashara.

Wachezaji wengine wa Yanga SC ambao ni majeruhi, ni kama ifuatavyo:

Kibwana Shomary Jumatatu ataanza mazoezi na wenzake.
Khalid Aucho yupo hatua ya pili ya utimamu na anaendelea vizuri akiwa fiti zaidi ataingia hatua ya tatu ya mazoezi kisha atajiunga na wenzake.
Zawadi Mauya anaendelea vizuri.
Yao Kouassi ana majeraha ya nyama za paja mpaka sasa hivi kwa mujibu wa ripoti ya madaktari ni asilimia 50 x 50 kuivaa Mamelodi Sundowns.
Pacome Zouzoua, ana shida ya goti lakini madaktari wa Ivory Coast walimuhitaji kuwa nae karibu zaidi hivyo taarifa za mchezaji huyo zitatoka baada ya mrejesho wa madaktari wetu na wa Ivory Coast.

Odds kubwa, kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti ni njia rahisi ya kukupa mtonyo mrefu. Ingia mchezoni hapa.

Mchezo huo unachukuliwa kwa hisia tofauti na mashabiki pamoja na wapenzi wa shoka kutokana na wapinzani wa Yanga, Mamelodi Sundowns wanapewa nafasi kubwa ya ushindi licha ya kwamba, Wananchi wana kikosi kizuri na wanaweza kupata matokeo katika dimba la Mkapa siku hiyo ya Jumamosi. Bashiri mechi hii kupitia Meridianbet odds kubwa, machaguo kibao na bonasi za kasino pia unazipata.

Acha ujumbe