“NYIE TULIENI TU” ni kauli ya Mastaa wa Simba walivyotoa ahadi mbele ya kikao kizito kilichoitishwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi na Rais wa Heshima wa Simba, Mohammed ‘Mo Dewji’ kabla ya jioni ya leo Julai 8 kuanza sfari ya kwenda Ismailia, Misri kujiandaa na msimu mpya wa mashindano 2024/25. Jisajili hapa kuwa wa kwanza kushinda Mamilioni ya Meridianbet kila siku.
Klabu ya Simba inaondoka kwenda Misri kuanza safari mpya ya kimageuzi chini ya Bilionea, Mo Dewji aliyerudi na jeuri akisajili kikosi kizito na kushusha benchi la ufundi kutoka Afrika Kusini chini ya Fadlu Davids ambalo nalo pamoja na wachezaji walifanya kikao kizito na Bodi ya Wakurugenzi kuwekana sawa.
