Kocha msaidizi wa klabu ya Simba Suleiman Matola ambaye alienda kuchukua kozi fupi ya kutafuta leseni A ya ukocha kupitiia shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika CAF arejea ndani ta Simba.

Kocha Matola amemaliza kozi yake ambayo alikua akisomea kwa muda wa siku kumi na kurejea ndani ya klabu ya Simba na majukumu yake kama kawaida huku akifanyia kazi kile ambacho alikisomea darasani kwa muda aliokua njeya timu.matolaKocha huyo baada ya kumaliza kozi yake fupi inaelezwa atakaa ndani ya klabu ya Simba kwa muda wa miezi mitatu kisha atarejea kumalizia kozi nyingine ambayo itamchukua muda wa siku kumi kama mwazo. Baada ya kumaliza kozi hiyo sasa ni wazi atatunukiwa leseni A ya CAF.

Matola atakua na uwezo wa kua kocha mkuu na kusimama kwenye bechi la ufundi la klabu yeyote kwenye michuano ya CAF atakapomaliza kozi yake ya pili, Kitu ambacho klabu ya Simba ilikua inakihitaji kutoka kwa kocha huyo.

Klabu ya Simba ina mpango wa kuwaendeleza wachezajii wake wengine ukocha ambao ni waandamizi ndani ya timu ambao ni Erasto Nyoni na nahodha John Bocco ambao kwasasa wamechukua inaelezwa wamechukua diploma ya awali kupitia shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF.

 

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa