Mara baada ya kujiunga na wenzake kambini Yanga,mshambuliaji wa timu hiyo Fiston Mayele ameongeza mzuka ndani ya timu hiyo jambo ambalo limeibua shangwe kubwa ndani ya kambi hiyo huku wenye timu yao wakisema kuwa wamekwisha.

Fiston Mayele juzi Jumatatu alirejea rasmi nchini na kujiunga moja kwa moja katika kambi ya timu hiyo inayoendelea kufanyika Avic Town Kigamboni.

Baada ya Mayele kutua ndani ya kambi hiyo,sasa ni rasmi Yanga watakuwa wamekamilisha jeshi lao kwajili ya msimu ujao kutokana na mastaa wengine wa timu hiyo wapya tayari kutua katika kambi ya timu hiyo kama Lomalisa Mutambala,Aziz Ki,Lazarous Kambole na Gael Bigirimana.

Mara baada ya kurejea ndani ya timu hiyo Fiston Mayele alisema kuwa sasa ni muda rasmi wa kuanza maandalizi ya msimu ujao huku akiahidi mafanikio kwa msimu ujao zaidi ya msimu uliomalizika.

“Tayari ni muda wa kuanza kazi,baada ya mapumziko sasa nimerejea rasmi kwaajili ya kupambana ,hii inaonyesha kuwa msimu mpya tayari umeshaanza huku nikiwa na matumaini makubwa ya kufanya vizri kwa msimu ujao zaidi ya msimu uliomalizika,”alisema mchezaji huyo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa