Mayele Kinara wa Mabao NBC Primia Ligi

Mshambuliaji wa Yanga Fiston Kalala Mayele ndiye anashikilia nafasi ya kwanza kwa wachezaji wenye mabao mengi katika ligi kuu ya NBC Primia Ligi mpaka sasa akiwa ameshaweka kambani mabao 10.

 

Mayele Kinara wa Mabao NBC Primia Ligi

Mayele amefikisha idadi ya mabao hayo juzi baada ya kutupia mabao mawili kwenye mchezo wao walipokuwa wakimenyana dhidi ya Dodoma Jiji na kujikusanyia pointi zao tatu muhimu ambazo zinazidi kuwaweka kileleni hadi sasa.

Baada ya Mayele, anayefuata kwenye mbio za ufungaji ni mshambuliaji wa Simba Mosses Phiri ambae nae baada ya kutupia kimyani mabao 2 alifanikisha kufikisha mabao yake nane akiwa amezidiwa mabao mawili tu na kinara.

Yanga inazidi kuimarika kadri siku zinavyozidi kwenda ikiwa imefikisha “Ubeaten” ya 49 hadi sasa huku hapo kesho ikitafuta ya 50 watakapomenyana dhidi ya Ihefu ambao ndio wanaoshikilia mkia mpaka sasa.

Mayele Kinara wa Mabao NBC Primia Ligi

Mshambuliaji huyo mabye amekuwa hatari anatafuta tuzo ya mfungaji bora ambayo aliikosa msimu uliopita mbele ya mshambuliaji wa Geita Gold George Mpole kwa bao moja pekee na msimu huu anaangaliwa kwa jicho jingine kama atabeba kiatu.

Yanga ambayo ipo chini ya Nasredine Nabi wapo kilelenikwenye msimamo wa Ligi kuu kutetea taji lao la msimu uliopita huku wakiwa na michezo miwili mkononi na wakiwa na pointi 32.

Mayele Kinara wa Mabao NBC Primia Ligi


Je wewe hucheza Kasino Mtandaoni na umekuwa ukijiuliza ni mchezo gani rahisi na mzuri kwa ushindi? Basi Usihangaike Aviator ni rahisi zaidi kucheza na kushinda, kingine cha zaidi ni kwamba Aviator Bonanza imerudi tena Cheza zaidi ujiweke kwenye nafasi ya kushinda Samsung A23.

BONYEZA HAPA KUCHEZA

 

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.