Klabu ya Mbeya City baada ya kutoa sare ya kufungana akiwa nyumbani kwake, hapo kesho anatarajia kumkaribisha Geita Gold nyumbani kwake kwaajili ya kucheza mchezo wao wa Ligi majira ya saa 8:00 mchana.

 

Mbeya City Uso kwa Uso na Geita Gold

Mbeya City ambayo imeanza vizuri ligi wapo nafasi ya 6 kwenye msimamo baada ya kucheza michezo 11 kwenye Ligi wakiwa wameshinda michezo minee, wakienda sare mara tano na kupoteza michezo miwili tu wakijikusanyia pointi 17.

Wakati kwa upande wa Geita Gold ya Geita wao wapo nafasi ya 7 kwenye Ligi wakiwa wamecheza michezo 12, wameshinda michezo minne, sare tano na kupoteza mara tatu huku wakiwa pointi sawa na Mbeya ambazo ni 17.

Mbeya City Uso kwa Uso na Geita Gold

Kinachowatofautisha wao ni kwenye mechi za kupoteza huku mwenyeji akiwa amepoteza mbili wakati mgeni yeye amepoteza tatu, pia Mbeya ana mchezo mmoja mkononi.

Mechi ya mwisho kukutana timu hizi mbili Geita alishinda ugenini kwa bao moja kwa bila na kujichukulia pointi tatu muhimu. Je huu unaweza kuwa mchezo wa Mbeya City kulipiza kisasi au Geita ataendeleza ubabe?

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa