KOCHA Msaidizi wa Mbeya City, Anthon Mwamlima baada ya timu yake kupoteza mechi dhidi ya Singida Big Stars kwa mabao 2-1 ametoa lawama kwa waamuzi wa mchezo huo.

Mchezo huo wa ligi kuu mzunguko wa pili ulipigwa jana jumapili kwenye Uwanja wa Liti, Singida.

Mbeya City, Mbeya City Yalia na Waamuzi, Meridianbet

Akizungumzia matokeo hayo, Mwamlima amesema kuwa: “Kwanza tunamshukuru Mungu mchezo umemalizika salama licha ya kwamba tumepoteza.

“Mimi huwa sipendi kuzungumza lakini ili mpira wetu ili ukuwe inabidi kuwepo na umakini sana kwa wale ambao wanasimamia sheria za soka.

“Unaposajili wachezaji ambao unaamini wana uwezo waache wacheze mpira lakini sisi kwa upande wetu tumeona mapungufu yetu hivyo tutaenda kwenye uwanja wa mazoezi kufanyia marekebisho.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa