Mbrazil kocha wa Simba ampa zawadi Kibu

Kocha mpya wa Simba, raia wa Brazil Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amempa zawadi kiungo mshambuliaji, Kibu Denis baada ya kuonyesha kiwango kizuri.

Simba inaendelea na mazoezi nchini Dubai kwa ajili ya kujiandaa na mchezo ujao wa ligi dhidi ya Mbeya City.

Mbrazil kocha wa Simba ampa zawadi Kibu

Ofisa Habari wa Simba, Ahmed Ally amesema kuwa kocha Robertinho alimpa zawadi hiyo Kibu Denis jana baada ya mazoezi.

“Kikosi chetu kinaendelea na mazoezi hapa nchini Dubai, wachezaji wote tuliokuja nao wapo fiti na kila kitu kipo sawa.

“Tunayofuraha kwa mchezaji wetu Clatous Chama kuongezeka kwenye kikosi chetu ambapo aliungana nasi hapa Dubai jana akitokea kwao Zambia.

Mbrazil kocha wa Simba ampa zawadi Kibu

“Tukio lililotokea hapa kambini jana baada ya mazoezi ni Kocha Robertinho kumpa zawadi Kibu Denis kutokana na kuwa na kiwango kizuri mazoezini na amesema utakuwa ni mwendelezo kwa yeyote atakayefanya vizuri.

“Kocha amesema ameangalia rekodi za Kibu za hivi karibuni ameona sio nzuri hivyo atakaa nae chini kwa ajili ya kumjenga kisaikolojia ili awe na kiwango kizuri.

Acha ujumbe