MCHEZAJI SIMBA AOMBA KUVUNJA MKATABA

IMEFAHAMIKA kuwa kiungo mshambuliaji kinda wa Simba, Jimmson Mwanuke amegoma kutolewa kwa mkopo katika klabu hiyo huku akishinikiza avunjiwe mkataba wake.SIMBASimba hivi karibuni ilielezwa kuwepo katika mipango ya kumtoa kwa mkopo kiungo, kabla ya dirisha kubwa la msimu huu kufungwa katika msimu huu Agosti 31, mwaka huu.

Kiungo huyo ni kati ya wachezaji ambao wamekosa nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha Mbrazili, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ tangu msimu uliopita.

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa, kiungo amegomea kutolewa kwa mkopo baada ya kikao cha muda mrefu kilichofanyika juzi Jumanne kati ya kiungo huyo na uongozi.

Aliongeza kuwa kiungo huyo amekubali kuondoka hapo Simba, kwa sharti la mkataba wake uvunjwe ili awe huru kwenda popote anapotaka kwenda kabla ya dirisha kubwa halijafungwa.

“Simba imefanya mazungumzo na mchezaji wake Mwanuke kwa ajili ya kumtoa kwa mkopo katika dirisha hili la usajili ambalo linatarajiwa kufungwa Agosti 31, mwaka huu.

“Katika mazungumzo hayo, Mwanuke amewaambia vongozi wa Simba, kuwa hayupo tayari kutolewa kwa mkopo, kama klabu inataka kuachana nae ivunje mkataba,” alisema mtoa taarifa huyo.SIMBAAkizungumzai hilo, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally alisema kuwa: “Taarifa zote za usajili wa wachezaji wapya, wakuachwa na kutolewa zipo kwa kocha wetu Robertinho, tusubirie muda ukifika litatolewa ufafanuzi.

Acha ujumbe